Ufafanuzi wa beberu katika Kiswahili

beberu

nominoPlural mabeberu

 • 1

  mbuzi dume.

 • 2

  mwanamume mwenye nguvu.

 • 3

  mtu anayetoa harufu mbaya.

 • 4

  taifa linalotawala nchi nyingine kiuchumi au kisiasa.

 • 5

  mtu anayeamini na kutekeleza siasa ya ubeberu.

Asili

Khi

Matamshi

beberu

/bɛbɛru/