Ufafanuzi wa bomba katika Kiswahili

bomba

nominoPlural mabomba

 • 1

  mwanzi mpana na mrefu wa chuma, plastiki au saruji unaochimbiwa ardhini kupitisha mafuta au maji.

  mfereji

 • 2

  mwanzi unaosimamishwa juu ya paa la nyumba, karakana au melini ili kutoa moshi nje.

 • 3

  chombo cha kutilia dawa mwilini mwa binadamu au mnyama ili kutoa uchafu k.v. sikioni, n.k..

  ‘Piga bomba’

 • 4

  mtambo wenye mwanzi wa chuma, n.k. na shikio la kutia maji sehemu ya chini kwenda sehemu ya juu k.v. kutoka kisimani.

 • 5

  chombo cha kusemea ili maneno yasikike mbali.

 • 6

  chombo cha kupulizia dawa ya majimaji ya kuua wadudu.

  ‘Bomba la kupigia dawa ya mbu’

Asili

Kre

Matamshi

bomba

/bɔmba/