Ufafanuzi msingi wa chacha katika Kiswahili

: chacha1chacha2

chacha1

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  (kinywaji, chakula, n.k.) geuka kuwa kikali.

  chachuka

 • 2

  kuwa na hasira.

  kasirika

 • 3

  Kibaharia
  kuwa na mawimbi makubwa na makali; kuchafuka kwa bahari.

 • 4

  endelea au zidi kufanya jambo kwa nguvu.

  ‘Fulani amechacha kunywa pombe siku hizi’
  chachawa, chaga, charuka

Matamshi

chacha

/t∫at∫a/

Ufafanuzi msingi wa chacha katika Kiswahili

: chacha1chacha2

chacha2

nominoPlural chacha

 • 1

  aina ya majani yanayoota kwenye sehemu zenye majimaji.

Matamshi

chacha

/t∫at∫a/