Ufafanuzi wa chochea katika Kiswahili

chochea

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lea, ~leana, ~lewa, ~sha, ~wa

 • 1

  sogezasogeza au gusagusa kwa kijiti.

 • 2

  sababisha ugomvi.

  chokoza, kasirisha, chipua

 • 3

  tia hamu au shauku ya kufanya kazi.

 • 4

  chuma tunda kwa kutumia ncha ya jiti refu lisilokuwa na kigoe kwa kulisukuma kwa ncha ya jiti hilo.

Matamshi

chochea

/t∫ɔt∫ɛja/