Ufafanuzi wa chukua katika Kiswahili

chukua

kitenzi elekezi~ana, ~lia, ~liana, ~lika, ~liwa, ~za

 • 1

  twaa kitu mkononi.

  twaa

 • 2

  ‘Chukua pesa hizi’
  pokea

 • 3

  fanya kuwa mali yako; enda na.

  ‘Chukua nguo’
  iba

 • 4

  beba mzigo kichwani, begani au kwenye gari la hamali.

 • 5

  kuwa na uvumilivu.

  stahimili, vumilia

 • 6

  tunza mtu asiyejiweza k.m. wazee.

  ‘Kua uje unichukue kama nilivyokuchukua’

 • 7

  tumia muda fulani.

  ‘Kazi hii itachukua saa mbili kumalizika’

 • 8

  ‘Nguo aliyovaa imemchukua’
  pendeza

Matamshi

chukua

/t∫ukuwa/