Ufafanuzi wa dawa katika Kiswahili

dawa

nominoPlural dawa, Plural madawa

 • 1

  kitu anachopewa mgonjwa, agh. huwa cha vidonge, majimaji au unga, ili kutibu ugonjwa alionao.

  maponyo

 • 2

  kitu kinachotengenezwa ili kuua wadudu au wanyama waharibifu.

  ‘Dawa ya mbu’
  ‘Dawa ya panya’

 • 3

  kitu kinachotumiwa kukomesha tabia fulani.

  ‘Dawa ya mtoto mkaidi ni kumnyima zawadi’

 • 4

  talasimu, amali, azima, hirizi, utabibu, uganga, majuni, tiba

Asili

Kar

Matamshi

dawa

/dawa/