Ufafanuzi wa dondoka katika Kiswahili

dondoka

kitenzi elekezi~ea, ~eana, ~eka, ~esha, ~ewa, ~wa

 • 1

  anguka kwa maji au kitu cha majimaji, tone baada ya tone.

  tona

 • 2

  anguka kwa kitu au mtu kutoka mahali pa juu.

  ponyoka

 • 3

  (ms) ingiwa na mahaba juu ya mpenzi mke au mume.

Matamshi

dondoka

/dɔndɔka/