Ufafanuzi wa fikicha katika Kiswahili

fikicha

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  weka katikati ya vidole au viganja viwili na kusugua.

  ‘Fikicha macho’
  ‘Fikicha nguo’
  fikinya, sugua

 • 2

  ondoa mbegu katika mashuke ya nafaka.

  pukusa

Matamshi

fikicha

/fikit∫a/