Ufafanuzi wa fimbo katika Kiswahili

fimbo

nominoPlural fimbo

 • 1

  kipande cha mti kinachotumiwa hasa kwa kumpigia mtu au mnyama.

  bakora, gongo, henzirani, mkwaju

 • 2

  kipande cha mti kinachochongwa kwa makusudi ya kushika mkononi na kutembelea, kupigia au kuchezea ngoma fulani.

  methali ‘Fimbo ya mbali haiui nyoka’
  mkongojo, asa

Matamshi

fimbo

/fimbÉ”/