Ufafanuzi wa fumbua katika Kiswahili

fumbua

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lia, ~liana, ~lisha, ~liwa

 • 1

  eleza siri au habari au jambo lililo gumu kufahamika.

  fichua

 • 2

  funua ili kuwa wazi.

  ‘Fumbua mkono’
  ‘Fumbua macho’
  ‘Fumbua mdomo’
  ‘Fumbua maana’
  ‘Fumbua fumbo’
  funua, fundua

Matamshi

fumbua

/fumbuwa/