Ufafanuzi wa goli katika Kiswahili

goli

nominoPlural magoli

 • 1

  mlango ulio kati ya milingoti miwili wa kufungia magoli katika mchezo k.v. kandanda, mpira wa mikono au mpira wa magongo.

  ‘Miti ya goli’

 • 2

  pete iliyotundikwa juu ya mlingoti ambamo mpira hutumbukizwa katika mchezo wa mpira wa vikapu, netiboli, n.k..

 • 3

  uingiaji wa mpira katika mlango, kikapu au pete katika michezo.

  bao, dungu, fora, nage

Asili

Kng

Matamshi

goli

/gɔli/