Ufafanuzi msingi wa haha katika Kiswahili

: haha1haha2

haha1

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  kula kwa haraka au kwa uroho; wania kwa pupa.

  papia, lapa

 • 2

  toa pumzi kwa kasi na shida k.v. baada ya kukimbia sana.

  hema

 • 3

  babaika katika kueleza jambo kwa kuwa na haraka ya kusema; shindwa kueleza jambo kwa sababu ya hofu au kuwa jambo lile ni la uongo.

Matamshi

haha

/haha/

Ufafanuzi msingi wa haha katika Kiswahili

: haha1haha2

haha2

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  shikwa na hasira juu ya jambo dogo.

  hangaika, sumbuka

Matamshi

haha

/haha/