Ufafanuzi wa hizi katika Kiswahili

hizi

kitenzi elekezi

 • 1

  fanyia mtu jambo asilolipenda.

  kirihi

 • 2

  vunjia mtu heshima.

  ‘Mwana amemhizi baba yake hadharani’
  aibisha, dhili, fedhehesha, tehemu, fedhehi, dunisha, adhiri

 • 3

  tia katika majanga au hatari.

Matamshi

hizi

/hizi/