Ufafanuzi wa hongo katika Kiswahili

hongo

nominoPlural hongo

 • 1

  malipo au zawadi anayotoa mtu ili kupata haki.

  rushwa, chai, chauchau, chirimiri, mlungula, kadhongo, chichiri, mvugulio, kiinikizo, kilemba

 • 2

  fedha au kitu anachopewa mtu ili kumshawishi atoe huduma fulani.

 • 3

  malipo yaliyokuwa yakitolewa kwa watawala wa kienyeji wa zamani ili kupata idhini ya kupita katika nchi zao.

  ushuru

Matamshi

hongo

/hɔngɔ/