Ufafanuzi msingi wa kama katika Kiswahili

: kama1kama2

kama1

kiunganishi

 • 1

  hutumika kujulisha mithili au mfanano wa kitu, jambo au mtu mmoja kwa kulinganishwa na mwingine.

  mithili, mfano, sawasawa, ja

 • 2

  hutumika pamoja na ‘nini’ kusisitiza jambo.

  ‘Mzuri kama nini’

 • 3

  huonyesha jambo lisilo na hakika.

  ‘Kama atakuja, utampa’

 • 4

  kuliko.

  ‘Afadhali kufa kama kuishi utumwani’

 • 5

  hutumika katika kukisia jambo.

  ‘Watu kama mia hivi’

Matamshi

kama

/kama/

Ufafanuzi msingi wa kama katika Kiswahili

: kama1kama2

kama2

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  bana kwa kila upande ili kutoa nje uowevu uliomo ndani, hasa katika kukamua matiti.

Matamshi

kama

/kama/