Ufafanuzi wa katibu katika Kiswahili

katibu

nomino

 • 1

  mtu anayefanya kazi za kuandika kumbukumbu na kuhifadhi maandishi ya shirika, kampuni au chama.

  mwandishi

 • 2

  ofisa au mfanyakazi anayepewa wadhifa maalumu na shirika, kampuni au chama.

  ‘Katibu myeko’
  ‘Katibu shakhsiya’
  ‘Katibu mahususi’
  ‘Katibu muhtasi’
  ‘Katibu mwenezaji’
  ‘Katibu mtendaji’