Ufafanuzi msingi wa kitovu katika Kiswahili

: kitovu1kitovu2kitovu3

kitovu1

nominoPlural vitovu

 • 1

  uzi wa mshipa ulioko kwenye tumbo unaounganisha mtoto na mama tumboni.

 • 2

  kovu lililoko katikati ya tumbo baada ya uzi wa mshipa huo kukatwa na kukauka.

Matamshi

kitovu

/kitOvu/

Ufafanuzi msingi wa kitovu katika Kiswahili

: kitovu1kitovu2kitovu3

kitovu2

nominoPlural vitovu

 • 1

  asili au chimbuko la kitu au mtu.

  ‘Kitovu cha lugha ya Kiswahili ni pwani ya Afrika Mashariki’

Matamshi

kitovu

/kitOvu/

Ufafanuzi msingi wa kitovu katika Kiswahili

: kitovu1kitovu2kitovu3

kitovu3

nominoPlural vitovu

 • 1

  kituo kikuu cha shughuli fulani k.v. biashara.

  ‘Arusha ni kitovu cha shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki’

Matamshi

kitovu

/kitOvu/