Ufafanuzi msingi wa kodi katika Kiswahili

: kodi1kodi2

kodi1

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa

 • 1

  panga nyumba au shamba kwa malipo fulani.

 • 2

  chukua kitu na kukitumia kwa malipo ya muda unaokitumia.

  ‘Kodi teksi’

Asili

Khi

Matamshi

kodi

/kOdi/

Ufafanuzi msingi wa kodi katika Kiswahili

: kodi1kodi2

kodi2

nomino

 • 1

  malipo kwa ajili ya kitu kilichochukuliwa au kupangwa na kutumiwa kwa muda.

  kiharara

 • 2

  fedha inayotozwa na serikali.

  ‘Lipa kodi’
  ‘Toza kodi’
  ‘Kodi ya mapato’
  ada

Asili

Khi

Matamshi

kodi

/kOdi/