Ufafanuzi wa mgeni katika Kiswahili

mgeni

nominoPlural wageni

 • 1

  mtu ambaye si mwenyeji wa mahali fulani.

  mweni, ajinabi

 • 2

  mtu aliyealikwa katika shughuli fulani.

  methali ‘Mgeni njoo, mwenyeji apone’
  methali ‘Mgeni ni kuku mweupe’
  methali ‘Mgeni pofu ingawa ana macho yake’

Matamshi

mgeni

/mgɛni/