Ufafanuzi wa mkondo katika Kiswahili

mkondo

nominoPlural mikondo

 • 1

  njia ya maji k.v. katika bahari, mto au ziwa inayopitisha maji kwa kasi na kwa nguvu.

 • 2

  njia isiyo ya kawaida inayofanywa na mtu au mnyama katika nyasi.

 • 3

  mchepuo k.v. katika madarasa, masomo, n.k..

 • 4

  njia ya mawimbi ya umeme au sauti inayowezesha kuvisafirisha vitu hivyo mpaka pale vinapohitajika.

Matamshi

mkondo

/mkɔndɔ/