Ufafanuzi msingi wa mwana katika Kiswahili

: mwana1mwana2

mwana1

nominoPlural wana

 • 1

  kiumbe aliyezaliwa na binadamu au mnyama.

  methali ‘Mwana wa nyoka ni nyoka’
  methali ‘Mwana wa yungiyungi hulewa, seuze wa mlimwengu’
  methali ‘Mwana mtukutu hali ugali mtupu’
  methali ‘Mwana akililia wembe mpe’
  methali ‘Mwana umleavyo ndivyo akuavyo’
  methali ‘Mwana wa mhunzi asiposana hufukuta’
  methali ‘Mwana kidonda, mjukuu kovu’
  methali ‘Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura’
  mtoto

Ufafanuzi msingi wa mwana katika Kiswahili

: mwana1mwana2

mwana2

nominoPlural wana

 • 1

  neno la heshima linalotumika kabla ya kutaja jina la mwanamke.

  ‘Mwana Fatuma’
  siti, nunu

Matamshi

mwana

/mwana/