Ufafanuzi msingi wa mwao katika Kiswahili

: mwao1mwao2

mwao1

nominoPlural myao

 • 1

  hali ya kuwa na habari; tendo la kufahamu jambo.

  ‘Habari hizi sina mwao nazo’

 • 2

  hali ya kushikilia jambo.

  ‘Tokea mzozo wetu na Hamisi basi imekuwa mwao’

Matamshi

mwao

/mwaɔ/

Ufafanuzi msingi wa mwao katika Kiswahili

: mwao1mwao2

mwao2

nominoPlural myao

 • 1

  vipande vya boriti vinavyotandazwa chini ili kupitishiwa mashua juu yake wakati wa kushusha mashua hiyo au jahazi.

  mhimili, chao

 • 2

  kipande cha mti kilichowekwa chini ya chombo ili shehena isipate maji.

Matamshi

mwao

/mwaɔ/