Ufafanuzi wa mzinga katika Kiswahili

mzinga

nominoPlural mizinga

 • 1

  kitu kirefu cha mviringo chenye uwazi ndani kinachotengenezwa kwa mbao au mti.

  ‘Mzinga wa nyuki’

 • 2

  chombo kinachotengenezwa kwa chuma chenye mwanzi mkubwa ambao hutumika kurushia risasi kwa nguvu zaidi kuliko bunduki.

  ‘Piga mzinga’

 • 3

  idadi ya ushindi wa mabao sita katika mchezo wa karata.

 • 4

  fremu ya ngoma ambayo huwambwa ngozi.

Matamshi

mzinga

/mzinga/