Ufafanuzi wa nchi katika Kiswahili

nchi

nominoPlural nchi

 • 1

  sehemu ya ardhi isiyofunikwa na maji.

  bara

 • 2

  sehemu ya ardhi katika ulimwengu iliyogawanyika kisiasa kwa mipaka na kutambulikana kwa taifa lake.

  ‘Nchi ya Tanzania’
  ‘Nchi ya Kenya’
  ‘Nchi ya Marekani’

Matamshi

nchi

/n ntʃi/