Ufafanuzi wa ndugu katika Kiswahili

ndugu

nominoPlural ndugu

 • 1

  mtu aliyezaliwa nawe kwa baba, kwa mama au kwa wazazi wote wawili.

 • 2

  mtu aliyezaliwa aliye wa ukoo mmoja na wewe.

  akraba, jamaa, akhi

 • 3

  rafiki mkubwa.

 • 4

  mtu unayeshirikiana naye katika shughuli za dini au siasa.

  methali ‘Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kapu ukavune’

Matamshi

ndugu

/ndugu/