Ufafanuzi msingi wa pakua katika Kiswahili

: pakua1pakua2

pakua1

kitenzi elekezi~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

  • 1

    teremsha mizigo kutoka kwenye chombo cha kusafiria k.v. meli au gari.

  • 2

    toa chakula kutoka chomboni kilimopikiwa na kukitia katika chombo kingine ili kuwa tayari kuliwa.

    ‘Pakua chakula’

Ufafanuzi msingi wa pakua katika Kiswahili

: pakua1pakua2

pakua2

kitenzi elekezi~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

  • 1

    hamisha kwa kukopi faili au data toka kwenye seva ya intaneti au mtandao hadi kwenye kompyuta ili mtumiaji aifanyie kazi.

Matamshi

pakua

/pakuwa/