Ufafanuzi wa pindua katika Kiswahili

pindua

kitenzi elekezi~ana, ~ka, ~lia, ~liana, ~liwa

 • 1

  geuza chini kuwa juu au nje kuwa ndani.

  ‘Pindua gari’
  ‘Pindua kikombe’
  ‘Pindua shati’
  funikiza, petua

 • 2

  chukua nafasi ya mwingine kwa kutumia hila au nguvu.

  ‘Pindua serikali’

Matamshi

pindua

/pinduwa/