Ufafanuzi wa pole! katika Kiswahili

pole!

kiingizi

  • 1

    tamko la kumliwaza mtu aliyefikwa na jambo baya k.v. kuumia au kufiwa.

    ‘Pole kwa kufiwa!’

  • 2

    neno la kumpoza mtu anayefanya kazi au aliyetoka safarini au kazini.

    ‘Pole kwa safari!’

Matamshi

pole!

/pɔlɛ/