Ufafanuzi msingi wa puliza katika Kiswahili

: puliza1puliza2

puliza1

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  toa upepo kwa nguvu kupitia kinywani au kwenye pampu.

  ‘Puliza moto’
  vuvia

 • 2

  toa dawa kwa manyunyu kwa kutumia bomba.

  ‘Puliza dawa ya mbu’

Matamshi

puliza

/puliza/

Ufafanuzi msingi wa puliza katika Kiswahili

: puliza1puliza2

puliza2

kitenzi elekezi~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  legeza mshipi kidogo baada ya samaki kujisimbika kwenye ndoana.

  ‘Puliza mshipi’

Matamshi

puliza

/puliza/