Ufafanuzi msingi wa rahisi katika Kiswahili

: rahisi1rahisi2

rahisi1

kitenzi elekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  punguza thamani.

  dunisha, tweza, beza

Asili

Kar

Matamshi

rahisi

/rahisi/

Ufafanuzi msingi wa rahisi katika Kiswahili

: rahisi1rahisi2

rahisi2

kivumishi

 • 1

  -enye bei ndogo; -enye thamani ndogo.

  sahili, chewale, bahasa, nyara, mboga, chee

 • 2

  -siyo taabu kufanyika.

  ‘Hesabu hizi ni rahisi sana’

Asili

Kar

Matamshi

rahisi

/rahisi/