Ufafanuzi msingi wa ringa katika Kiswahili

: ringa1ringa2

ringa1

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha, ~iana, ~iwa, ~wa

 • 1

  tia madaha wakati wa kutenda jambo, k.v. wakati wa kwenda au kucheza ngoma; tia maringo.

 • 2

  jiona bora kuliko wengine; kuwa na kiburi.

  jiona, shaua, shana, jibodoa, jifaragua, jivuna, takabari

Matamshi

ringa

/ringa/

Ufafanuzi msingi wa ringa katika Kiswahili

: ringa1ringa2

ringa2

kitenzi elekezi~ia, ~ika, ~isha, ~iana, ~iwa, ~wa

 • 1

  tia msichana mimba kabla ya kuoana.

  ‘Paulo amemringa Roda’

Matamshi

ringa

/ringa/