Ufafanuzi msingi wa ruka katika Kiswahili

: ruka1ruka2ruka3ruka4

ruka1

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  toka chini na kwenda juu.

 • 2

  toka mahali kumoja hadi kwingine kwa kupitia hewani, agh. kwa kutumia mabawa au chombo k.v. eropleni, n.k..

  methali ‘Kila ndege huruka kwa ubawa wake’
  puruka

Ufafanuzi msingi wa ruka katika Kiswahili

: ruka1ruka2ruka3ruka4

ruka2

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  pita juu ya kitu bila ya kukikanyaga.

  ‘Nilikuwa nimelala, akaja akaniruka’
  kiuka, tambuka

Ufafanuzi msingi wa ruka katika Kiswahili

: ruka1ruka2ruka3ruka4

ruka3

kitenzi sielekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  kataa kukubali jambo ambalo unalifahamu.

  kana

Ufafanuzi msingi wa ruka katika Kiswahili

: ruka1ruka2ruka3ruka4

ruka4

kitenzi sielekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  (nguo) kuwa fupi kuliko ilivyokuwa mwanzo.

  paa, rudi

Matamshi

ruka

/ruka/