Ufafanuzi wa shabaha katika Kiswahili

shabaha

nominoPlural shabaha

 • 1

  kitu kilichowekwa ili kulengwa na kupigwa k.v. kwa mshale, bunduki au mkuki.

  lengo, dango

 • 2

  uwezo au uhodari wa kupiga kinacholengwa.

  ‘Huyu hana shabaha’

 • 3

  matarajio ya matokeo ya kitendo fulani.

  ‘Ulipofanya hili, shabaha yako ilikuwa ni nini?’
  makusudi

Asili

Kar

Matamshi

shabaha

/∫abaha/