Ufafanuzi msingi wa shinda katika Kiswahili

: shinda1shinda2shinda3

shinda1

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~ika, ~isha, ~wa

 • 1

  kuwa wa kwanza katika mashindano.

  ‘Katika mechi ya leo hakuna timu iliyoshinda’

 • 2

  kuwa zaidi ya.

  ‘Huyu amemshinda ndugu yake kwa unene’
  pita, fyokocha, kulula

 • 3

  lemea

 • 4

  faulu katika jambo.

  ‘Ameshinda mtihani’
  fuzu, vota

Matamshi

shinda

/∫inda/

Ufafanuzi msingi wa shinda katika Kiswahili

: shinda1shinda2shinda3

shinda2

kitenzi sielekezi~ana, ~ia, ~ika, ~isha, ~wa

 • 1

  enda na kukaa mahali kutwa nzima.

  ‘Dada yangu leo amekwenda kushinda kwa shangazi’

 • 2

  kuwa mahali au katika hali fulani kwa muda wa siku nzima.

  ‘Leo nimeshinda na njaa’
  ‘Nimeshinda bila ya kufanya kazi yoyote, kutwa nzima sikufanya kazi’

Matamshi

shinda

/∫inda/

Ufafanuzi msingi wa shinda katika Kiswahili

: shinda1shinda2shinda3

shinda3

kivumishi

 • 1

  -siyojaa.

Matamshi

shinda

/∫inda/