Ufafanuzi wa simama katika Kiswahili

simama

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  kuwa wima kwa kutegemea sehemu ya chini, agh. miguu ya mtu, kitu au kitako cha kitu.

  inuka, dinda, ima

 • 2

  acha kuendelea kutenda jambo fulani.

  ‘Gari limesimama kwa sababu limekwisha petroli’

 • 3

  kuwa sawa bila ya kuwa na mapindo au mapando.

  ‘Amelipiga pasi shati lake mpaka mikono yake imesimama upanga’

Matamshi

simama

/simama/