Ufafanuzi wa simamisha katika Kiswahili

simamisha

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~iwa, ~wa

 • 1

  fanya kilichokaa kiinuke na kuwa wima.

 • 2

  zuia jambo lililokuwa likitendeka lisiendelee kufanyika; fanya kitu kilichokuwa kikienda k.v. gari au mashine, kisimame.

  ‘Serikali imesimamisha ujenzi wa barabara’
  sitisha, kimu, zuia

 • 3

  teua mtu agombee kiti fulani cha siasa, chama, n.k..

 • 4

  simika

Matamshi

simamisha

/simami∫a/