Ufafanuzi wa stakimu katika Kiswahili

stakimu

kitenzi sielekezi

 • 1

  fanya mahali fulani kuwa ndiyo maskani.

  ‘Hapa ndipo ninapostakimu’

 • 2

  kuwa na hali nzuri ya maisha.

  stawi

 • 3

  thibitika kuwa ni kweli.

  ‘Habari zimestakimu kwamba kesho ni sikukuu’

Asili

Kar

Matamshi

stakimu

/stakimu/