Ufafanuzi wa tamu katika Kiswahili

tamu

kivumishi

  • 1

    -enye ladha ya sukari.

  • 2

    -enye ladha ya kuridhisha kinywani.

    ‘Nyama hii ni tamu sana’

  • 3

    -enye kufurahisha.

    ‘Muziki huu mtamu sana’

  • 4

    (kwa maji) maji yasiyo ya chumvi k.v. ya mto.

    baridi

Asili

Kar

Matamshi

tamu

/tamu/