Ufafanuzi wa tawala katika Kiswahili

tawala

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa

 • 1

  kuwa na mamlaka juu ya nchi fulani au maisha ya watu.

  ‘Wakoloni walitawala Afrika’
  dabu, tamalaki, miliki, wika

 • 2

  mudu kitu au jambo kwa kiwango cha juu.

  ‘Mwalimu anaitawala fani ya ushairi’

Asili

Kar

Matamshi

tawala

/tawala/