Ufafanuzi wa teleza katika Kiswahili

teleza

kitenzi sielekezi~ea, ~eka, ~esha

 • 1

  serereka kama mtu anapokanyaga mahali penye tope au palipo pororo.

  ‘Usipite hapo panateleza’
  sepetuka, serereka, pepesuka

 • 2

  enda kwa ulaini k.v. kamasi, ute, grisi au mafuta.

  nyiririka

 • 3

  kuwa na hali ya kunyiririka au ulaini unaoweza kusababisha kuserereka.

 • 4

  fanya kosa dogo kwa bahati mbaya.

 • 5

  agaa, ponyoka

Matamshi

teleza

/tɛlɛza/