Ufafanuzi msingi wa tena katika Kiswahili

: tena1tena2tena3

tena1

kiunganishi

 • 1

  neno linalounganisha mambo mawili au zaidi juu ya kitu kimoja kwa wakati mmoja.

  ‘Juma ni mrefu tena mnene’
  kadhalika, vilevile, pia

Matamshi

tena

/tɛna/

Ufafanuzi msingi wa tena katika Kiswahili

: tena1tena2tena3

tena2

kielezi

 • 1

  neno linaloonesha kurudiwa kwa jambo au tendo kwa mara nyingine.

  ‘Jana alikuja, leo atakuja tena’

Matamshi

tena

/tɛna/

Ufafanuzi msingi wa tena katika Kiswahili

: tena1tena2tena3

tena3

kiingizi

 • 1

  neno linalothibitisha jambo, agh. ambalo halikutegemewa liwe hivyo.

  ‘Juma alikuwa anakusumbua, tena amekulipa pesa zako!’

Matamshi

tena

/tɛna/