Ufafanuzi wa twanga katika Kiswahili

twanga

kitenzi elekezi~ana, ~ia, ~iana, ~ika, ~isha, ~iwa, ~wa

 • 1

  ponda kitu k.v. mahindi katika kinu kwa kutumia mchi ili kutoa maganda katika punje.

  ‘Twanga mpunga’
  funda, ponda, pwaya, chakacha

 • 2

  saga, seta

 • 3

  piga vibaya kwa ngumi.

Matamshi

twanga

/twanga/