Ufafanuzi wa ubichi katika Kiswahili

ubichi

nominoPlural ubichi

 • 1

  hali ya kutokuwa mbivu; kutoiva.

 • 2

  hali ya kutoiva baada ya kupikwa.

  ‘Ubichi wa nyama ulinifanya nisiwe na hamu ya kuendelea kuila’

 • 3

  hali ya kutokuwa kavu.

  ‘Ubichi wa nguo baada ya mvua kumnyeshea ndio uliomzidishia homa’
  uchepechepe

 • 4

  hali ya kutopevuka; mwanzomwanzo wa jambo, mtu au kitu.

  ‘Kinachowavutia wengi ni ubichi wa yule kijana’

Matamshi

ubichi

/ubit∫i/