Ufafanuzi wa zaidi katika Kiswahili

zaidi

kielezi

 • 1

  iliyopita kiwango cha kawaida au iliyopita vitu vingine kwa sifa k.v. ukubwa au uzuri.

  ‘Shati hili ni kubwa zaidi’
  ‘Mwaka huu kuna joto zaidi ya mwaka jana’
  sana, kayaya, mno

 • 2

  iliyo ya ziada au nyongeza.

  ‘Nipe maji zaidi’
  -ingine

Asili

Kar

Matamshi

zaidi

/zaIdi/