Ufafanuzi msingi wa zindua katika Kiswahili

: zindua1zindua2

zindua1

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~lika, ~liwa, ~sha

 • 1

  toa katika bumbuazi au usahaulifu.

  tanabahisha

 • 2

  toa mtu katika kutofahamu jambo; fanya mtu awe na habari juu ya jambo fulani.

  ‘Lau si fulani kuja kunizindua , haya mambo ningeyafanya ovyoovyo’

Matamshi

zindua

/zinduwa/

Ufafanuzi msingi wa zindua katika Kiswahili

: zindua1zindua2

zindua2

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~lika, ~liwa, ~sha

 • 1

  anzisha au fungua kitu kwa mara ya kwanza ili kianze kutumika.

  ‘Barabara hii mpya atakayeizindua ni Waziri wa Ujenzi’

Matamshi

zindua

/zinduwa/