Ufafanuzi msingi wa chambua katika Kiswahili

: chambua1chambua2

chambua1

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa, ~ana

 • 1

  tenga vitu vilivyoshikana pamoja kati ya kifaacho na kisichofaa.

  ‘Chambua pamba/karafuu’

 • 2

  soma maandishi kwa makini na kuyagawanya katika sehemu mbalimbali ukionyesha yaliyomo, mambo mazuri na udhaifu wa mwandishi.

  hakiki

Matamshi

chambua

/t∫ambuwa/

Ufafanuzi msingi wa chambua katika Kiswahili

: chambua1chambua2

chambua2

kitenzi elekezi~ka, ~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa, ~ana

 • 1

  tangaza makosa ya mtu huku ukimtukana.

Matamshi

chambua

/tʃambuwa/