Ufafanuzi msingi wa dharau katika Kiswahili

: dharau1dharau2

dharau1

kitenzi elekezi~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

  • 1

    kosa kuthamini mtu au kitu; vunjia mtu heshima.

    bera, pukurusha, fedhehi, beua, deua, beza, tweza, nyarafu

  • 2

    kosa kutia maanani.

    ‘Dharau mahakama’
    bekua, kefya, puuza

Ufafanuzi msingi wa dharau katika Kiswahili

: dharau1dharau2

dharau2

nominoPlural dharau

  • 1

    tabia ya kutothamini au kutoheshimu mtu au kitu; tabia ya kupuuza.

    dhalala, puruzai

Asili

Kar

Matamshi

dharau

/ðarawu/