Ufafanuzi wa diriki katika Kiswahili

diriki

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  jipa moyo wa kutenda jambo fulani.

  jasiri

 • 2

  kuwa wa kwanza katika kufanya jambo fulani.

  takadamu, anza, wahi, ongoza, tangulia

 • 3

  tulia mahali pamoja.

  makinika

 • 4

  fanya jambo kwa wakati kabla ya kuharibika; wahi kuokoa kitu kabla hakijaharibika.

Matamshi

diriki

/diriki/