Ufafanuzi wa funua katika Kiswahili

funua

kitenzi elekezi~ana, ~lia, ~liana, ~lika, ~lisha, ~liwa

 • 1

  ondoa kifuniko au kitu kilichowekwa juu ya kitu au mahali; weka wazi kilichofunikwa.

  ‘Funua chungu’
  gubua, fumbua, fundua, fichua, futua

 • 2

  eleza kwa maneno yanayofahamika kwa urahisi; ondoa shaka.

  eleza

 • 3

  ‘Funua mbawa’
  tandaza

Matamshi

funua

/funuwa/