Ufafanuzi wa husu katika Kiswahili

husu

kitenzi sielekezi~ia, ~ika, ~isha

 • 1

  kuwa na fungamano au uhusiano na; kuwa na ujamaa na.

  ‘Fulani ananihusu’

 • 2

  andikia mtu fungu; toa fungu kwa; toa hisa ya azimu.

 • 3

  pasa, juzu

Asili

Kar

Matamshi

husu

/husu/